Habari za Punde

Mhe Mansoor alipochangia kwenye Kongamano la nafasi ya Zanzibar



Mh Mansoor Yussuf Himid amewataka baadhi ya watu kutokuwa wepesi kwa kuwanyooshea vidole wenzao kwa sasa ni wakati wa kuzungumza kweli tena bila ya uwoga hasa katika mustakbali wa wazanzibar na nchi yao.
 
Amesema wanaosimama na kusema hadharani kuwa mkiutaka msiutake muungano ndio huu huu kuwa wanakosea kwani hakuna mwenye haki ya kumlazimisha mtu juu ya anachokitaka mwenyewe.
Iweje leo baadhi ya viongozi wawatishe wananchi juu ya mustakbali wa nchi yao
 
Amewataka Wazanzibari kutokukubali kurudishwa walipotoka kwa sasa ni kwenda mbele na sio kurudi tena nyuma na amewaomba viongozi wenzake kuwa ni mabalozi juu ya hili kufikisha ujumbe kwa wengine wasiojua nini cha kufanya kwa sasa juu ya nchi yao ili waweze kuungana na wazanzibari wanaotaka kupumua na muungano huu.
 
Pia amesema yeye haoni tatizo kwa mwananchi kutoa maoni yake anayoyataka juu ya muungano anaoutaka mwenyewe.
 
Amewataka wananchi kutokuvunjika moyo na wajitokeze kwa wingi sana kutoa maoni yao wakati wa tume ya kukusanya maoni itakapopita waende kwa wingi sana kwenye mchakato wa kutoa maoni muda utakapofika ili waweze kuikomboa Zanzibar yao.

Stori kwa hisani ya Hamed Mazrui via Face book

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.