Habari za Punde

Dereva wa Sheikh Farid aongea


Akizungumzia mkasa wa kupoteza kwa Sheikh Farid, Dereva aliyempakia, Said Omar alisema alitumwa kununua na kupeleka umeme nyumbani kwao na ndipo alipomuacha Sheikh huyo hapo eneo la Mweni hapo akiwa na watu wakizungumza naye ndani ya gari aina ya Noah lakini hakuwahi kuchukua namba zake na pia hakuweza kuona sura za watu hao kwa kuwa walikuwa katika gari yenye vioo vyeusi.
 
Akizungumza kwa khofu mbele ya waandishi wa habari huko Mbuyuni Mjini Unguja, muda mfupi baada ya kumaliza sala ya Ijumaa Said alisema kwamba baada ya kurejea nyumbani alimfuata ambapo hakumkuta tena jambo ambalo lilimtia wasiwasi na kurejea kuongea na wake zake nyumbani kwamba Sheikh Farid haonekani.
 
  Naye kwa upande wake Naibu Amir wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI) Azzan Khalid Hamad anasema taasisi za kiislamu zinaamini kwamba Sheikh Farid bado yupo mikononi mwa jeshi la polisi.


Sheikh Azzan alisema bado wataendelea kumtafuta licha ya kuwa serikali inaonekana kushindwa kufanya hivyo ambapo wametoa wametoa muda wa saa 26 hadi hapo kesho iwapo hajaonekana watachukua hatua wenyewe ya kumtafuta.
 
Aidha aliwataka waumini wa dini ya kiislamu kuendeleza amani katika kipindi hicho na kuacha kujiingiza katika makundi ya kihuni ambapo alisema kumetokea vijana wenye kufanya vurugu na baadae kusingiziwa Uamsho.
 
  Sheikh Azzan alisema kukamatwa kwa Sheikh Farid ni juhudi za kuwarejesha nyuma wazanzibari katika kudai haki yao ambapo alisema wapo watu ambao hawataki kuona serikali ya umoja wa kitaifa ikiendelea na ndio wanafanya kila njia ya kuvuruga amani nchini.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.