Habari za Punde

Wanaume Zanzibar kupewa likizo ya uzazi


Na Mwantanga Ame 

 WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, amesema mipango inaandaliwa kuhakikisha akina baba wanapatia likizo ya uzazi, pindipo wake zao wanapojifungua. 

 Waziri huyo alisema msingi wa hatua hiyo utasaidia ulezi wa wazazi wawili baina ya mama na baba mara tu wanapojaaliwa kupata mtoto. 

 Waziri huyo alileza hayo jana ofisini kwake mjini hapa alipokuwa akitoa taarifa ya serikali ikiwa ni maadhimisho ya siku watu duniani. 


 Kwa miaka kadhaa hivi sasa wafanyakazi wa kike katika serikali ya Zanzibar wamekuwa wakifaidika na mpango wa likizo ya uzazi kwa kupata mapumziko ya kipindi cha mienzi mitatu mara tu wanapojifungua na kupewa muda wa saa nzima ya kwenda kumpatia mtoto maziwa ya mama. 

 Alisema katika kuimarisha huduma za uzazi wa mpango na malezi kwa watoto wataozaliwa na watumishi wa umma, serikali inakusudia kuchukua hatua ya kuwapa likizo ya uzazi wanaume ili kumsaidia mama ulezi kwa mtoto aliyezaliwa. 

 Alisema hivi sasa utaratibu wa likizo ya uzazi upo kwa upande mmoja tu ambao wamekuwa akipewa mwanamke, lakini hata hivyo bado imeonekana haujaweza kuleta tija kutokana na wanaume kujiona kama sio sehemu ya kuisaidia familia katika kipindi hicho. 

 Kutokana na hali hiyo waziri huyo alisema wizara hiyo kwa kushirikiana na wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, tayari imeanza kuandaa kanuni ili kina baba nao wapatiwe likizo (siku tano za kazi) la uzazi ili kumsaidia mama na mtoto aliezaliwa. 

 “Hatua hii itasaidia kuondokana na ile dhana kwamba suala la afya ya uzazi linamhusu mama pekee, lakini hatua hii inategemewa iwe chachu ya kuwashirikisha kina baba katika harakati zote za huduma ya afya ya uzazi na mtoto”, alisema waziri huyo.

 Aidha waziri huyo alisema katika kuliunga mkono hilo, serikali kuanzia bajeti ya mwaka huu 2012/13 imetenga fungu maalum kwa ajili ya huduma za afya, upatikanaji wa vifaa na dawa mbali mbali. 

 Alisema lengo la serikali kuchukua uamuzi huo ni pamoja na kurahisisha upatikanaji huduma ya afya uzazi kwa kinamama, kupunguza vifo vya kina mama na watoto na kuimarisha ustawi wa wananchi kwa ujumla. 

Waziri huyo alisema bado kuna mwamko mdogo kwa wananchi wa Zanzibar katika suala zima la utekelezaji wa uzazi wa mpango kutokana na idadi ya watu kuendelea kuongezeka. 

 Alisema idadi ya watu hapa Zanzibar inakadiriwa kufikia watu milioni 1.3 ikiwa ni ongezeko la kasi ya asilimia 3.1 kwa mwaka ambapo idadi ya watu katika kila kilomita moja ya mraba imefikia watu 496 mwaka 2011.

 Alisema sababu kubwa zinazochangia ongezeko hilo ni pamoja na kiwango kikubwa cha uzazi cha wastani wa watoto watano kwa kina mama wenye umri wa kuzaa, kiwango kidogo cha matumizi ya njia za uzazi wa mpango na ndoa za mapema. 

 Waziri huyo alisema kwa mujibu wa utafiti wa demografia na afya wa mwaka 2009/10, kiwango cha matumizi ya njia za uzazi wa mpango Zanzibar kimefikia asilimia 12.4, kiwango ambacho ni kidogo na hivyo huchangia kuwepo kwa wastani mkubwa wa kuzaa hapa Zanzibar. 

 Akiendelea alisema kwa upande wa Tanzania bara kiwango hicho cha CPR kimefikia asilimia 27 ambayo pia bado haijakidhi haja inayokusudiwa. Alisema taarifa za Wizara ya Afya Zanzibar pia zinaonyesha kwamba bado kuna muamko mdogo wa matumizi ya njia za muda mrefu za uzazi wa mipango, ikilinganishwa na zile za muda mfupi. 

 Kutokana na hali hiyo waziri huyo alisema jamii inahitaji kuelimishwa zaidi juu ya kuwepo na ubora wa njia hizo za muda mrefu katika kupanga uzazi salama kwa akina mama. 

 Alisema mwaka 2010, watu 3,390 ndio waliojitokeza kupatiwa njia za muda mrefu za uzazi wa mpango sawa na asilimia 3.9 ikilinganishwa na watu 84,414 ( asilimia 96.1) waliorodheshwa katika matumizi ya njia za muda mfupi za uzazi wa mpango. 

 Akifafanua zaidi waziri huyo alisema watu walio wengi wameorodheshwa kwenye matumizi ya sindano (asilimia 71) na vidonge (asilimia 19.4) na juhudi zaidi zinahitajika ili kudhibiti hali hiyo na hatimae kuwe na uwiano mzuri baina ya ongezeko la idadi ya watu na ukuaji wa uchumi.

 Waziri huyo alisema changamato ziliopo serikali itajitahidi kuona inazifanyia kazi likiwemo suala la kuwapa huduma bure mama wajawazito ndani ya kipindi cha ulezi wa mamba zao. Kaulimbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ni “UPATIKANAJI WA HUDUMA ZA AFYA YA UZAZI KWA WOTE” ambayo inaendana na lengo la melenia la 5b lisemalo ifikapo mwaka 2015 “Huduma za Afya ya Uzazi kupatikana kwa wote”.

9 comments:

  1. Natumai Mh. Waziri ataacha tabia ya kuzaa na wanawake tofauti tofauti na kutokua na muda wa kuwaangalia hao watoto zaidi ya kuwatumia pesa za matumizi. Malezi ya mtoto sio pesa tuu, mapenzi ya wazazi wote wawili ni muhimu kwa ustawi wa mtoto.

    ReplyDelete
  2. Siku tano ndio nini, mimi naona huyu Waziri anafanya mchezo,angalau angalaifanya hiyo miezi mitatu kwa baba vile vile. Hapa Canada, mtu akipata mtoto yeye na mkewe wanapewa mwaka mmoja. Ikiwa mama hafanyi kazi, baba anaramba mwaka mzima na ikiwa wotw wanafanya kazi wanaweza kugawana miezi sita sita au anaweza kuchukuwa mmoja wao mwaka mzima.

    ReplyDelete
  3. Mhe. Waziri mwisalm safi hana watoto kwa mama tofauti. Ana binti zake watatu tu

    ReplyDelete
  4. sijui lini sisi Waznz tutakuwa serious on issues!!!
    Anonymous who posted at 9:41am...what you said is off point...kama huyo waziri alikuzalisha au alimzalisha dada yako (ndugu yako) peleka malalamiko sehemu husika!
    Anonymous wa saa 2:03pm are you serious kweli? Canada isnt Zanzibar! have you tried to put your concern kwa mume mwenye wake wanne ambao kila mwaka mke mmoja anazaa?

    ReplyDelete
  5. wewye ulitetuma 9:41 uwe na adabu kwa viongozi wako, huachi maneno yasiyo na mana

    ReplyDelete
  6. anon wa 3:23 yaelekea humfahamu kabisa mh. hehehee utabaki tuu hivyo hivyo eti ana binti watatu tuu.

    ReplyDelete
  7. hehehe weye, ndie usiyemfahamu haswa mhe. ndio nye mtu akipata hamushi kumdalilisha, haya weye au nduguyo mezalishwa wangapi

    ReplyDelete
  8. Anaejiheshimu atapewa heshima anayostahili, asiyejiheshimu hata awe na wadhifa gani hatoheshimika. Napita tuu hapa jamani.

    ReplyDelete
  9. DU!... Partenity leave mwaka mzima? na nchi maskini kama hi yetu si bora wahusika wache kazi?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.