Habari za Punde



Mhe Abraham Mwampashe Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar akizinduwa Kitabu cha Ripoti ya Haki za Binaadamu kilichoandikwa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, kushuto  Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chris Maina Peter, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani.

Mhe Jaji Ambraham Mwampashe akionesha Kitabu cha Ripoti ya Haki za Binaadamu baada ya kukizinduwa hoteli ya bwawani, kulia Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo hicho Profesa Chris Maina Peter, Kamishna wa Haki za Binadamu Tanzania Zanzibar Zahor Ali Khamis na Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraj Mpatani. 

Mhe Jaji Abraham Mwampashe, akifunguwa  uzinduzi wa Kitabu cha Ripoti ya Tanzania ya Haki za Binaadamu iliotolewa na Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar, uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa hoteli ya bwawani Zanzibar.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Profesa Chris Maina Peter, akizungumza machache kuhusiana na uzinduzi huo wa Ripoti ya Haki za Binadamu wa uzinduzi wake hoteli ya bwawani.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar Harusi Miraj Mpatani, akisoma baadhi ya kurasa za Ripoti ya Kitabu hicho kwa Wananchi waliohudhuria uzindu huo na kufafanua baadhi ya maelezo ya ripoti hiyo.

Wananchi na Wanasheria na Viongozi wa Ngos wakipitia ripoti hiyo wakati Kaimu Mkurugenzi Harusi Mpatani akisoma baadhi ya vipengele vya ripoti hiyo. 
 

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.