Habari za Punde

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Akutana na Viongozi wa Dini na Waandishi Zanzibar

Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali. 
Waziri Dk. Nchimbi  akisisitiza jambo katika Mkutano wake na Viongozi wa Dini  kuzungumzia Vurugu zilizotokea juzi katika mitaa ya mji wa Zanzibar.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.
Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar.  
Viongozi wa Jumuiya  za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena  ikaharibu  Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.
Mwandishi wa habari wa Nipashe Mwinyi Sadala akiuliza swalim katika Mkutano huo.uliowashirikisha Viongozi wa Jumuiya za Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuziungumzia vyurugu hizo..
Mwandishi wa Redio HIT FM, Jacob, alipota fursa ya kuuliza, katika Mkutano huo na Waziri wa Mambo ya Ndani Dk. Nchimbi.    
Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza  nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya ZATI  Zanzibar Abdulsamad, amesema yeye amefarijika kwa ujio wa Waziri wa Mambo ya Ndani na IGP,na amelitaka jeshi la Polisi kuzuiya fujo kama hizi zisitokea tena katika Visiwa vya Zanzibar ambavyo huzoretesha shughuli za Kitalii ikizingatiwa wakati huu ni msimu wa Utalii ikizingatiwa Zanzibar ni moja ya nchi zilizokuwa na Vivutio vya Utalii.  



SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar.  

3 comments:

  1. cha msingi ni kujua msingi wa ttzo na sio kujadili result za ttzo, watu tujifunze kusolve mattzo sio kuzipa viraka kila siku.

    Kura ya maoni is a key to the problem, na sijui why hawa wawakilishi wanashindwa kusema kwamba wananchi wanataka kura ya maoni kwanza kisha ndo mtajadili huo muungano. lakin ni baada ya kura ya maoni kujulikana km unatakiwa au hautakiwi tena.
    Tuwache kuwalazimisha watu mambo ambayo hawayataki. Na ni lazma kura ya maoni iitishwe zanzibar kwanza. hakuna sbb ya viongozi kuogopa matokeo na kwann muogope matokeo hali ya kua haijuilikan kama huo muungano unatakiwa znz au hautakiwi?

    ReplyDelete
  2. Wakati huyu Mussa anachaguliwa kamishna hapa Z'bar, watu wengi walipata matumaini kwamba sasa tumepata mtu mzuri msomi na muwajibikaji, matokeo yake..mambo yanaharibika!..hivi kweli mpaka aje Nchimbi na Mwema ndio polisi wafanye kazi?..wahuni wanaharibu mali za watu!

    Mimi zamani nikiambiwa Wazanzibari hawakusoma nilikua sikubali na nakasirika sana lkn hatimae nimethibisha!
    Hivi inakuwaje watu waliosoma kutumia vikundi vya dini kupeleka mbele ajenda zao za kisiasa?

    Niliwahi kusema hapa sku moja, historia inaonesha vikundi vya dini havijawahi kutoa madai hata kama ni ya haki yakakubaliwa huku nikieleza mifano ya Takiban, al shabab nk. watu wakajibu kwamba UWAMSHO wanaungwa mkono na marekani..haya angalia leo hii?

    Wazungu 'wanatufitinisha' kila kona, ukifungua mitandao ya nje utatamani kutalia..kama wewe sio UWAMSHO ..manaake hawa ukiwaambia utalii utaathirika hawaelewi, dunia itatutenga hawaelewi..wao wapo tuu!

    Kinachonishangaza ni kwamba WAZANZIBARI waliosoma wanashindwa ku'counter' upotoshaji wa habari zinazohusu machafuko ya Z'BAR..kwenye mitandao.. wao wapo tuu! kama jana muhuni mmoja JOHN MASHAKA alitoa makala kwa kiingereza kwenye MICHUZI BLOG watu 71 walichangia, nadhani wazenji ni 5 tu na wengi hawana hoja za msingi ni matusi au hoja nyepesi, nyepesi tuu!.."hatutaki muungano!" "wabara wende zao!"

    Kwa kweli " ujinga ni nusu ya ukafiri" sasa hivi inaonesha wazi kua miaka yetu 40 ya elimu bila malipo tuliichezea inauma sana kuona hata waziri wa habari anashindwa kuvikemea vyombo vya habari vya bara kwa upotoshaji mfano JUZI KWENYE TAARIFA YA HABRI YA ITV kufungua tuu" VURUGU -Z'BAR, MAKANISA YACHOMWA MOTO! wakati kanisa lenyewe moja, lengo
    ni kutifitinisha kwa WAKRISTO WA BARA!

    Ndugu zanguni tupelekeni watoto wetu skuli kwa mgarama yeyote ile!..Z'bar bado hata tukiipata hiyo nchi kwa mtindo huu itakuja kutushinda.

    ReplyDelete
  3. UMEONA...EEH? ALAFU MSEME HAMCHAGULIWI KTK VYEO VIKUBWA VYA MUUNGANO HAYA KAMA HUYO MSHKAJI ANASHINWA KUTULIZWA GHASIA ZA WATU MILIONI NA LAKI MBILI, AKICHAGULIWA KAMISHNA HUKU BARA SI WATAMUOWA?

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.