Habari za Punde

Serikali Yapiga Marufuku Mikusanyiko Yote isiyokuwa na Kibali

Na Juma Mohammed,MAELEZO

Zanzibar Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imepiga marufuku mikusanyiko ya aina yoyote ikiwemo mihadhara ya aina mbalimbali ambayo hajapata kibali cha Serikali.

 Akitoa taarifa ya Serikali,Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais ,Mohammed Aboud Mohammed amesema mbali na suala hilo,pia imewataka wananchi kuheshimu sheria.

 Waziri Aboud amesema pia Serikali imeliagiza Jeshi la Polisi kuwatafuta na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wale wote waliohusika na fujo zilizotokea jana na leo katika mji wa Zanzibar. “Serikali inakemea vikali vitendo vyote vya hujuma na uharibifu wa mali zilizofanywa katika taasisi za umma,Dini na watu binafsi” Alisisitiza Waziri huyo.



 Serikali imetoa mkono wa pole kwa wale wote walioathirika na vurugu hizo ikiwemo Taasisi na wananchi kwa ujumla na imeahidi kuchukua hatua kali dhidi ya wale wote waliohusika kufanya vurugu hizo. Katika hatua nyengine, Waziri Aboud alisema Serikali inawaomba wazazi kuwadhibiti vijana wao kutojiingiza katika vitendo vya viovu ikiwa pamoja na vurugu,hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa atakayekiuka sheria na taratibu za nchi. “Tunawaomba wananchi waendelee na shughuli zao kama kawaida na Serikali itaendelea kuhakikisha amani na usalama wakati wote” Alisema Waziri Aboud katika taarifa yake aliyosoma mbele ya vyombo vya habari katika studio za Shirika la Utangazaji Zanzibar.

 Katika taarifa yake,wananchi pia wameombwa na Serikali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za wahalifu na wale wote wanaotaka kuvunja amani katika jamii. “Tunawaomba wananchi kushirikiana na Serikali kwa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi pale ambapo itaonekana zipo dalili za uvunjifu wa amani katika maeneo yao” Alitoa wito Waziri Aboud.

 Katika taarifa hiyo,Serikali imewakumbusha viongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislam na Jumuiya nyengine kufuata taratibu ikiwa wanataka kufanya mikutano au mihadhara inayojadili suala zima la kuandikwa kwa katiba ya Jamhuri ya Tanzania. Awali, Waziri huyo alisema Serikali iliwaita viongozi wa uamsho kuzungumzia namna bora ya kufanya mikutano inayozungumza wanaotaka kuendesha mijadala ya katiba mpya kwamba watalazimika kufuata sheria na taratibu za Tume ya Katiba iliyoundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

12 comments:

  1. ww bwege sana toka zilipoanza fujo hujaweka habari leo baada ya serikali kutoa kauli zao sizo ndio unaweka tulia nazo 2

    ReplyDelete
  2. Brother hiyo sio lugha ya kumfahamisha muandishi, ilikuwa tumuombe awe uptodate na habari zake, tuwache jazba Wazanzibari tutumie akili na hikma zaidi katika kutatua matatizo yetu na inshaalla M/Mungu atakuwa pamoja nasi........Amin

    ReplyDelete
  3. SMZ imechelewa sana kuwapiga marufuku hawa wahuni!'ukicheza na mbwa mwisho anakufata msikitini' kilichotokea Z'bar nilikua nakitarajia!

    Hawa wahuni wameachiwa mpaka wameharibu jina na sifa ya Z'bar nje ya nchi!..nilikua naangalia mtandao mmoja hapa tayari taarifa zimeshasambaa kwamba islamists wanataka kugeuza tropical paradise into Afghan of East Africa.

    Sote ni wazanzibari na sote ni waislamu lakini uwamsho wanataka kutuharibia nchi!

    ReplyDelete
  4. Hawa wanotukana wengi ni memba wa MZALEDO.NET
    Huwa wanapitapita humu kupiga chabo ndio AL SHABAB wenyewe hao!..tuwasamehe bure tu!

    ReplyDelete
  5. hii blog naomba uibadilishe jina na wewe ni mlowezi mnafik blog nyingi za tanzania zimeweka masuala yanayohusu zanzibar wewe kutokana na uzembe ujinga uliokujaa na asili yako umeona ufiche kinachoendeleya znz

    ReplyDelete
  6. kunawasenge wanawalaumu muamcho ni wazanzibar ni haki yao hawakuanza wao kaanza mzee karume mzee jumbe babu dorado kila mzanzibar kinda kindaki anaumwa na uzanzibar nyinyi watanganyika moja tu ndiye mwenye akili MTIKILA muliobaki vichwa vimejaa mavi unabaki mkilawitiwa na mafisadi hata janjuwi wapi munapoelekeya na wewe mapara nikibaraka hujuwi utendalo sawa na mfu jiandaye na kurudi kwenu tanzanyika aliyekuleta znz mtafute akuoneshe wapi ulipotokeya huna sifa uchungu utu ustarabu wa kizanzibar

    ReplyDelete
  7. huyu mwenye hii blog ni kelbu kama huyo mohammed aboud washezi wakubwa nyie hapa hakieleweki mpaka tupate zanzibar yetu iwe huru kutoka kwa hii mishenzi wa kitanganyika.

    ReplyDelete
  8. Mimi nasema kwa upuuzi na misimamo ya mamna hii ya kubagua watu kuwachomea majengo yao ya ibada na kuwatishia kuwarudisha kwao jambo ambalo ni kinyume hata na uislamu, Allah atawalaani na hamfanikiwi!

    Kama nyinyi mnaomba dua na sisi tunaomba vile vile Mungu ni wetu sote
    Mtapata laana kama walivyopata wazee wenu kina ALI MUHSIN, NA MOH'D SHAMTE walioishia ughaibuni!

    Hapa haondoki mtu, kuun.. faya kuun, tunaahidi tutawalinda ndugu zetu katika imani kama vile wachole, wazaramu, wamakonde, wandengereko na wengine mpaka dakika za mwisho!..kama mtu anasema yeye ni Mz'bari ajue kwao/kwakwe ni nyumbani kwake tuu hapa kila mtu anakaa kwake/kwao!

    ReplyDelete
  9. Zanzibar tunaelekea wapi tuwache mambo ya UBAGUZI Mwenyezimungu hapendi, Wa-Zanzibari tunaongelea Uislamu wa nchi tukumbuke hakuna nchi ya Kiislamu ila Wa-Islamu tupo kote Duniani na Allah kashusha Dini kwa kila Mwanadamu ya Kiislamu, tukumbuke hata Bara kuna Waislamu wenzetu na ndomana Allah akasema Wao wana Dini Yao na Sie tuna Dini yetu leo tunafanya Tabia za Makafiri na sie au za wa Oman wanavyozarau jamaa zetu bila kuijuwa dini yetu ipo vipi katika maswala ya ubaguzi? Tufanye vitu kwa Amani tukumbuke tuna jamaa zetu kibao nje ya nchi na hata Tanzania wana maduka Bara na wanaishi vizuri na imani ya dini inaendelea. Wa-Zanzibar tuwe na Subra inshaAllah mwenyezimungu ni Mmoja atatufungulia Dua zetu na kuishi kwa Amani na kuacha hizi tabia nakufanya Sunna za mtume anavyopenda tufanye, watu wakitukana sio na sisi ndio tutukane. Alhidaaya.com

    ReplyDelete
  10. Najua kuna watu wanaumwa sana lakini Wazanzibar ni haki yao kufanya wanavyofanya,wameshaonewa vya kutosha na Tanganyika. Suala hapa sio ubaguzi bali ni watu kudai haki yao. Sasa jamaa watu kudai haki yao ni kosa ?Halafu kuna watu wanadai oh' Wazanzibar wavute subra, mimi nauliza mpaka lini ? Hivi nyinyi munaowatetea serikali ya Tanzania kwa lipi kubwa walilowafanyia Wazanzibar ? Nakupeni mfano mmoja tu pale ilipozama meli ya MV.SPICES TAKRIBANI masaa kumi na mbili hakuna hata uwokozi uliuofanywa,hakna headcopta ya serikali iliokuja pale kuokoa watu, hakuna Nchimbi waziri wa bara pale, hakuna mabalozi waliofika pale,leo hii Wazanzibar wanadai Nchi yao second tu ,mabalozi,mawaziri wa bara wameshafika, hii ni kuonesha kwamba Wazanzibar hawana lao jambo wametawaliwa na bara.Sasa ni hivi ikiwa kuna watu wanahisi kuwatesa watu ndio watafanakiwa kuwatuliza watu wasidai haki yao, basi watizameni Syria hivi sasa,yemen, tunisia,Misri baadae mutapata jibu.

    ReplyDelete
  11. waliochoma kanisa si uamsho ni vijana wa kitanganyika wa maskani za CCM wakishirikiana na Usalama wa Taifa na kuwasingizia Uamsho..Mashahidi ni watu wanaoishi mitaa ya kariakoo ndio walivyosema hivyo wao ni mashahidi waliona hiyo kitu wakati inatendeka.....Wallahi hatutorudi nyuma hii ni nchi yetu WAZANZIBARI Hakuna cha smz wala MTANGANYIKA yeyote yule tutakae msikiliza...na kitu chechote kile kibaya Jeshi la Tanganyika litakalofanya katika nchi yetu ya Zanzibar mujue kuwa kila kitu kitapatikana Record zake na tunazifikisha katika Ofisi za Vitengo vya Haki za Binadamu Duniani kote (Human Right watch) kama kawaida yetu, na tutazidi kuujulisha ulimwengu hali ya kisiasa inavyokwenda hapa Zanzibar.

    HATURUDI NYUMA MPAKA KIELEWEKE...JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA!!!

    ReplyDelete
  12. Wallah nyie viongozi wa Zanzibar swalini misikitini na wengine kama kawaida munaoabudu mabaa akina mohammed aboud jueni haya ni maisha ya kupita tu,wengi wetu makaburi tunayachungulia tutakwenda kusema vipi kwa mola wetu

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.