Habari za Punde

Operesheni Kuwasaka Wahalifu wa Vurugu Yaendelea

Na Juma Mohammed,MAELEZO

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) imesema operesheni ya kuwasaka wahalifu walihusika na vurugu za wiki iiliyopita inaendelea na Serikali haitakuwa na msalia mtume kwa yeyote aliyehusika na vurugu hizo.

Akizungumza katika mkutano na viongozi wa dini katika ukumbi wa Kanisa la Pentekoste Tanzania lililopo Kariakoo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais,Mohammed Aboud Mohammed alisema Serikali imesikitishwa na kitendo kilichotokea cha vurugu na uchomaji wa nyumba za ibada,Makanisa.

“Hizi ni njama za makusudi, nataka nisemawazi kwamba watu hawa wametangaza mapambano na Serikali,tutawashughulikia ipasavyo” Alionya Waziri Aboud.

watu waliofanya vurugu Zanzibar sasa watakiona kwani wametangaza mapambano na Serikali, itawashughuliki popote walipo.

Waziri Aboud alisema kwamba waumini wa dini zote wamekuwa wakiishi kwa upendo na maelewano makubwa kwa miaka mingi ambapo ustahamilivu wa kidini upo kwa hali ya juu katika Visiwa vya Unguja na Pemba.

“Mie nakumbuka nilipokuwa nakaa kule Shangani kwa mfano mwezi wa Ramadhani utakuta tunapelekeana vyakula,waislamu wanapeleka kwa wakristo na hata siku ya sikuuu ya Idd el fitr tunasherehekea pamoja,huwezi kubagua yupi mkristo yupi muislam” Alisema Waziri hyo.

Alisema Serikali inawapo pole waumini wa makanisa yaliyochomwa moto na kuwaahidi hatua kali zitachukuliwa dhidi ya wale wote waliohusika.

Akizungumza katika mkutano huo,Mkuu wa Jeshi la Polisi,Inspekta Jenerali, Said Mwema alisema Polisi imejipanga kimkakati kukabuiliana na wale wote watakaofanya au kuchochea ghasia.

“Tunaendelea kudhibiti hali,doria kama kawaida na pia tumeweka ulinzi maalum katika nyumba za ibada tumezijumuisha katika sehemu muhimu za ulinzi kwa kipindi hichi” Alisema IGP Mwema.

IGP Mwema alisema pia ameunda timu maalum ya kikosi kazi ambacho kinajumuisha maafisa kutoka Idara ya Upelelezi Makao Makuu Dar es Salaam kuchunguza matukio ya vurugu hizo na kuwachukulia hatua watakaobainika.

Alisema katika mkutano huo pia jumla ya watu 46 wamekamatwa jana(juzi) na kati ya hao 43 wamefikishwa mahakamani jana Mjini Zanzibar wakikabiliwa na tuhuma mbalimbali.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja,Abdallah Mwinyi Khamis alisema Serikali ya Mkoa wake imesikitishwa mno na vitendo vya ghasia na uchomaji wa makanisa moto.

Mkuu huyo wa Mkoa alisema uvumilivu wa kidini ni jambo la msingi sana na anaamini waliofanya vurugu na kuchoma baadhi ya makanisa moto sio waumini wa dini ya kiislamu bali ni wahalifu.

“Tujiulize jamani, hivi kweli muumini wa kiislam anaweza kwenda kuvunja baa na kasha kuanza kunywa pombe? Hawa sio waislam …hapa kuna jambo,tutawachunguza kubaini chanzo na wanaohusika na kadhiaa hii” Alisema Mkuu huyo wa Mkoa.

Akithibitisha uvumilivu wa kidini uliokuwepo Zanzibar tangu enzi na enzi,Mkuu wa Mkoa alitoa stamp ya Serikali ya Kikoloni iliyopambwa kwa picha za misikiti na makanisa wakati wa utawala wa Kisultan chini ya himaya ya Uingereza yenye ujumbe wa uvumilivu wa kidini Zanzibar.

“Stamp hii iliyokuwa imetolewa na Serikali ya Kiingereza wakati ule inathibitisha kwamba Zanzibar hakuna tatizo la waislamu na wakristo,huu jamani ni ushahidi tunashangaa leo wanatoka watu wanachoma moto kanisa” Alisema.

Alitoa mfano wa namna wananchi Zanzibar walivyokuwa wakiishi kwa upendo na mshikamano wa maziko ya aliyekuwa Waziri Mwandamizi katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,marehemu Brigedia Jenerali,Adam Mwakanjuki,idadi ya waislamu mazikoni ilikuwa kubwa kuliko ya dini nyengine.

“Mbali na hili la mwenzetu Mwakanjuki, mimi mwenyewe niliombwa na Skuli ya Kanisa St Joseph kusomesha, walikuwa na upungufu wa walimu,Wizara ya Elimu ikaniteuwa mie nienda kusomesha,nimeishi nao vizuri,hawakunitenga …mimi ndio mwalimu wa mwanzo muislam kusomesha skuli ya wakristo hapa Zanzibar” Aliongeza Mkuu huyo wa Mkoa.

Katibu Mkuu wa Makanisa ya Pentekoste Tanzania, Askofu David Mwasota aliishukuru Serikali kwa kuwaunga mkono na kuwa pamoja nao kitendo ambacho kinathibitisha dhamira njema ya Serikali na viongozi kwa ujumla.

Askofu Mwasota alisema kesho(leo) watafanya mkutano wa madhehebu yote ya kidini kuzungumzia kadhia hiyo mkutano ambao utafanyika katika Kanisa la Pentekoste Kariakoo Unguja.

Mkuu wa Dini ya Kiislam katika Ofisi ya Mufti Mkuu Zanzibar, SheikhThabit Noman Jongo ameshangazwa na watu wanaochoma moto makanisa na kuwafafanisha watu hao kuwa ni wahalifu na Serikali iwachukuli hatua kali kwani waislam hawana ugomvi na wakristo.

5 comments:

  1. Kwanini hii mikutano ifanyike kwenye makanisa kwani hakuna kumbi nyengine.Hii inaonesha wazi kuwa Kanisa ndio linaongoza Serikali na nyie mnaojiita viongozi wa kiislamu mnakubali kuingia makanisan.Haishangazi kwani tushaona Maraisi wetu wanakuwa mstari wa mbele hata kwenye maszishi ya wakiristo pamoja na kuweka mauwa na kupinda magoti mbele ya maiti.INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RAAJIUUN.

    ReplyDelete
  2. washenzi wakubwa nyie msokuwa na haya nyie mumeenda kwa Makafiri wenzenu kupanga mikakati mengine ya kuwaangamiza Wazanzibari sio, MAKANISA YAMECHOMA NA VIJANA WA MASKANI ZA CCM WAKISAIDIWA NA USALAMA WA TAIFA,TUNALIJUA HILO SISI SIO WAJINGA KIASI HICHO MNAVYOZANIA.

    Vatican City ni moja ya kitengo kinachopanga njama za kuiangamiza Zanzibar kwa kuwatumia maaskofu wa kitanganyika kama hamujui basi Habari ndio hiyo na hawatowaachia wazanzibari kabisa mpaka wafanikiwe njama zao za kuiondoa
    dini yetu ya kiislam na mida zetu za kizanzibari katika visiwa vyote...kwa sababu tayari wameshafanikiwa kuithibiti dini ya kiislam na waislamu wenyewe katika mwambao wa pwani yote kuanzia Mombasa,lamu, bagamoyo, na sehemu nyingi tu nyengine sasa wanazidi kasi kuimaliza Zanzibar wafungi misheni zao!!
    JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR KWANZA
    MAFISADI WOTE WASIOITAKIA KHERI ZANZIBAR YETU MUNGU ATA KUANGAMIZENI INSHALAH

    ReplyDelete
  3. NDIO MR Aboud uzi huo huo lakini kumbuka bado kwamba iko siku utaingia kaburini, sasa huo uwaziri wako na ukubwa wako hajashinda Firauni leo hii yuko wapi ? Twakumbushana ulua huo una mwisho wake lakini dini ya m/mungu na nguvu zake hazina kikomo.

    ReplyDelete
  4. Shaka imeniingia juu yako unaeandika maoni Kama uko usingizini, unajuwa hata jinsi ulivyopatikana. Kama Hunan adabu kiasi hicho ni dhahiri wazazi walipitikiwa. M/Mungu(subhana hu wataala) atakuswamehe wewe na wazazi wako

    ReplyDelete
  5. Lazma tukubali, serikali ilikosea sana kuruhusu mihadhara ya UWAMSHO.
    Mimi nilikua najiuliza hivi jamani SMZ wapo au wako holiday?..waswahili walisema 'usipoziba ufa utajenga ukuta'..haya sasa!

    Ili dunia iamini kwamba SMZ 'hailei' vitendo vya namna hii, mambo mawili lazma yafanyike;

    1)Serikali ifanye iwezalo kuhakikisha inapambana na 'media propergander' zinazofanywa na Tanganyika pamoja na washirika wao wa nje na kueleza ukweli juu ya kile hasa kilichotokea Z'bar.

    2)Serikali kupitia vyombo vya sheria ihakikishe wale wote waliokamatwa kuhusiana na vurugu, wanafanyiwa upelelezi wa kina ili waweze kuwataja wahusiaka wengine na kwa pamoja wachukuliwe hatua kali za kisheria, iwe mfano kwa wengine!

    Mwisho kabisa, SMZ ihakikishe inasimamia vizuri mchakato wa katiba, ikiwa ni pamoja na fursa iliyotoka ya kujadili upya makubaliano ya muungano(Articles of union) ili hatimae tuwe na muungano imara na kuwanyima nafasi hawa maskini wa mawazo( UWAMSHO) wanaotaka kuvunja muungano kwa chuki ili wawatie watu mitihani..wenyewe hawa wanataka waamshwe ili wajue kua muungano ukivunjwa kwa chuki kama wao wanavyotaka, kutakua na uadui mkubwa baina ya nchi zetu ambao utaathiri mahusiano ya kisiasa, kiuchumi na kijamii, ambapo wao hawa hawatakua na msaada.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.