Habari za Punde

Maonesho ya Wafanyakazi Mei Mosi Viwanja vya Amani.


Mfanyakazi wa Shirika la  Posta Kanda ya Zanzibar Khamis Suwed, akitowa maelezo kwa mteja aliyefika katika  banda lao katika maonesho ya Wafanyakazi ya Mei Mosi,katika viwanja vya Amani nje,huduma hiyo  mpya inayotarajiwa kuzinduliwa hivi karibu nayojulikana kwa  City Urgent Mail.   
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Kanda ya Zanzibar, wakitowa maelezo kwa Wananchi waliotembelea banda lao huduma wanazotowa kwa wateja wao. 
Mwananchi akitia saini kitabu cha wageni, alipotembelea banda la Mamlaka ya  ya Uhifadhi Mji Mkongwe Zanzibar, ikionekana picha ya jengo la Betil la Ajaib. ni moja ya kivutio kwa waliotembelea banda hilo kaika maonesho hayo yanayomalizika leo katika viwanja vya Amani.   
Wananchi wakimsikiliza Mtaalamu wa Kilimo Zanzibar Tatu Seif, akitowa maelezo ya Vunza anayeharibu mimea hasa makuti ya  mnazi anayejulikana kwa jina la Chonga,   
Miti ya Matunda mbalimbali ikiwa katika banda la Kilimo ikioneshwa kwa Wananchi katika maonesho hayo Amaan.
Wanafunzi mbalimbali waliofika katika maonesho ya Wafanyakazi ya Mei Mosi wakiangalia jinsi ya Msaidi Daktari wa wanyama Mbaraka Nuhu, akimfanyika upasuaji wa kumfunga uzazi paka, banda la Mradi wa SWPA  World Society for the Protection of Animal. banda hili limekuwa kivutio kwa Wananchi na Wanafunzi kujionea jinsi ya ufungaji wa uzazi kwa paka Zanzibar.  

Mtaalam wa Kampuni ya Gas ya Orxy, akitowa maelezo ya utumiaji wa majiko ya gesi rahisi, kwamwananchi aliotembelea banda lao kujionea jinsi ya huduma ya gesi inavyofanya kazi kwa urahisi na kwa garama nafuu.  
Mfanyakazi wa Shirika la Umeme Zanzibar Simai Mohammed , akitowa maelezo kwa mteja aliyetembelea banda hilo jinsi ya matumizi ya mita za Tukuza zinavyofanya kazi na jinsi ya kuingiza fedha, wakati wa maonesho ya Wafanyakazi Mei Mosi yaliofanyika viwanja vya Amaan. 
Wakulima wa Ushirika wa Mbogamboga Zanzibar, Associotion of Vegetable and Fruit Growers of Zanzibar, wakionesha  mbogamboga wanazolima katika maonesho hayo.  
Mfanyakazi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA, akitowa  maelezo ya huduma za shirika hilo inazozitowa kwa wateja wake, na matumizi ya mita ambazo tayari wameshaaza kufunga kwa wateja wake na jinsi ya kufanya malipo kwa kutumia kusoma matumi katika mita hizo.  
Wananchi wakiangalia mazao ya Baharini katika Banda la Uvuvi walipofika kutembelea maonesho hayo.

Mfanyakazi wa Idara ya Malaria Zanzibar akitowa huduma ya kucheki malaria Wananchi wanaofika kutembelea banda lao katika maonesho hayo yanayofanyika katika viwanja vya Amaan nje.
Wanafunzi wa Chuo cha Utalii Maruhubi wakitowa huduma ya Nyama Choma wakiwa katika moja ya mafunzo yao, kwa Wananchi wanaotembelea maonesho hayo Amaani.  
 Mwalim wa Chuo cha Utalii Zanzibar akiwahamasisha Wananchi na watoto kwa maswali mbalimbali ya kuimarisha Utalii Zanzibar na vivutio vya utalii.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.