Habari za Punde

Mahafali ya 14 ya Madrasat Nuur Islamiyat ya Ukutani (Mskiti Barza)

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad. akihutubia katika mahafali ya 14 ya Madrasat Nuur Islamiyat ya Ukutani yaliyofanyika katika Skuli ya Haile Sellassie, mjini Zanzibar,kulia Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu na kushoto ni Mudir wa Madrasa hiyo Ustadh Khalid Mohd Mrisho.
   Baadhi ya wazazi, walezi na waalikwa mbali mbali wakihughuria maadhimisho ya sherehe ya Mahafali ya Madrasat Nuur yaliyofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.
 Wanafunzi wa Madrasat Nuur Islamiya ya Ukutani Zanzibar wakisoma Kasida katika Mahafali ya Madrasa hiyo yaliyofanyika skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.
 Wanafunzi wa kiume wa Madrasat Nuur Islamiya ya Ukutani Zanzibar wakisoma kasida katika sherehe za Mahafali ya Madrasa yao yaliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora wa Madrasatu Nuur Ukutani Ustadh Othman Omar Othman.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akimkabidhi zawadi Mwanafunzi Bora wa madrasa hiyo Ustadhat Safia Abdalla Hamad
  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu (wanaume) wa madrasa hiyo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.