Habari za Punde

CCM Yazinduwa Tovoti yake Mjini Dodoma.

 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akizinduwa Tovoti ya Chama cha Mapinduzi Mjini Dodoma jana.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa na Rais wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais Tanzania Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Rais wa Serekali ya Mapinduzi Zanzibar  Dk. Ali Mohamed Shein na Makamu Mwenyekiiti wa CCM Zanzibar, Dk Amani Abeid Karume, wakiangalia Tovuti  baada ya kuzinduliwa jana.  

 Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais Dk.Jakaya Mrisho
Kikwete,akifungua mkutano wa Siku moja wa Halamashauri Kuu ya
Taifa,CCM katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma jana,wengine
(kushoto)Mjumbe wa Kamati Kuu na Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed
Shein,Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais Mstaafu Dk Amani Abeid
Karume,(kulia) Katibu Mkuu wa CCM Taifa Willson Mkama.[Picha na
Ramadhan Othman,Dodoma.]

Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Tanzania,Dk.Mohamed Gharib Bilal,Waziri
Mkuu  Mizengo Pinda, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Vuai Ali Vuai na Katibu wa Oganaizesheni ya CCM Taifa, Asha Abdalla
Juma,wakuimba wimbo wa Chama cha Mapinduzi wakati
Mwenyekiti wa Chama akiingia  katika ukumbi wa Mkutano wa
White House, Mjini Dodoma kufungua kikao
cha Halmashauri Kuu ya Taifa CCM jana. .[Picha na Ramadhan
Othman,Dodoma.]

Wajumbe wa Halamashauri Kuu ya Taifa CCM,wakiwa
katika ukumbi wa Mkutano wa White House Mjini Dodoma,wakati kikao cha
siku moja kilichofunguliwa na Mwenyekiti wake Rais Dk.Jakaya M.Kikwete
jana. .[Picha na Ramadhan Othman,Dodoma.]

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.