Habari za Punde

Siku ya Wafanyakazi Mei Mosi Viwanja Ukumbi wa Salama Bwawani.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akipokea maandamano ya Wafanyakazi, katika sherehe za maadhimisho ya Mei Mosi yaliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Bwawani Zanzibar. 
Wafanyakazi wa wakipita mbele ya Mgeni Rasmin Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kutowa heshima zao katika sherehe za kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani huadhimishwa kila mwaka Mei Mosi.





Vijana wa Scout Zanzibar wakiwa katika hali ya Ukakamavu wakijumuika na Wafanyakazi wa Setta mbalimbali Zanzibar.


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiondoka  baada ya kupokea maandamano ya Wafanyakazi na kuelekea Ukumbi wa Mkutano kuzungumza na Wafanyakazi, katika sherehe za maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliofanyika Ukumbi wa Salama Bwawani. 
Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar, wakijumuika na Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali Zanzibar katika maadhimisho  ya Siku ya Wafanyakazi Duniani Kitaifa yamefanyika Zanzibar katika Ukumbi wa Salama Bwawani. 
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Ukumbi wa Salama Bwawani, kuadhimisha siku ya Wafanyakazi Duniani wakiungana na  Wafanyakazi wezao Duniani kote.  
Waziri wa Kazi Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika, Mhe Haroun Ali Suleiman akitowa maelezo machache kuhusu maendeleo ya Wizara yake kuboresha hali ya Kiuchumi kwa Wananchi na Wafanyakazi. wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.  
Mwakilishi wa ILO  Zanzibar, akitowa Salamu za Shirika la Kazi Duniani wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani kuwakumbuka Wafanyakazi waliojitolea kudai haki za Wafanyakazi Duniani.
Mkurugenzi wa ZANEMA, Zanzibar Salahi S Salahi, akisoma risala ya Waajiri katika kilele cha sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani. katika ukumbi wa Salama Bwawani. 
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Zanzibar Mwinyi Mohammed, akisoma risala ya Wafanyakazi katika ukumbi wa Salama Bwawani, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.   
Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia katika sherehe za Siku ya Wafanyakazi Duniani katika Ukumbi wa Salama Bwawani.
Viongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wakijumuika na Wafanyakazi wa Sekta mbalimbali katika Ukumbi wa Salama Bwawani kuadhimisha Siku ya Wafanyakazi Duniani. 
Viongozi wa Vyama Shirikishi vya Wafanyakazi Zanzibar, wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwahutubia katika ukumbi wa Salama Bwawani ikiwa nisiku ya Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa katika picha ya pamoja Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi na Wafanyakazi Bora wa Mwaka 2011 na 2012.

1 comment:

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.