Habari za Punde

Uzinduzi wa Maandalizi ya Ijitimai ya Kimataifa Zanzibar

 Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda na Mwakilishi wa Jimbo la Fuoni Thuwaiba Kisasi akipata maelezo ya majengo ya Kijiji cha Jitimai Fuoni kutoka kwa Katibu wa Jumuiya hiyo Mwalim Hafidhi, al;ipofika katika uzinduzi wa maandalizi ya Ijitimai.
Mwanafunzi akisoma Quran ikiwa ni ufunguzi wa maandalizi ya Mkutano wa Ijitimai ya Kimataifa inayotartajiwa kufanyuika katika mwezi wa saba, katika viwanja vya Ijitimai Fuoni Zanzibar.
Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda Thuwaiba Kisasi, akitowa nasaha zake kwa Wanawake wa  Kiislamu walioghudhuria mkutano wa uzinduzi wa maandalizi ya Ijitimai, uliofanyika katika viwanja vya Ijitimai Fuoni Markasi.
Mwenyekiti wa Ijitimai Amiri Mkuu Ali Khamis, akitowa maelezo ya maandalizi ya Ijitimai ya Kimataifa inayotarajiwa kufanyika mwezi wa saba 2012, katika viwanja vya Ijitimai Fuoni na kuwashirikisha Waislamu wa mbnalimbali kutoka nje ya Zanzibar.
Katibu wa Ijitimai Mwalim Hafidh, akitowa machache katika uzinduzi wa maandalizi yanayofanya na kamati mbalimbali ili kufanikisha Ijitimai hiyo.  

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.