Habari za Punde

Ubalozi wa India Wakabidhi Vifaa vya Masomo ya Sayansi

Balozi Mdogo wa India Dalip Singal amemkabidhi Waziri wa Elimu na mafunzo ya amali Ali Juma Shamhuna vifaa mbali mbali vya masomo ya sayansi vyenye thamani ya dola laki moja za kimarekani ili visaidie kupunguza kero ya uhaba wa vifaa vya masomo ya sayansi hapa Zanzibar.

Vifaa ambavyo vimekabidhiwa kwa ajili ya kusaidia masomo ya Biologia, Kemia na Physikia vitasaidia kupunguza tatizo hilo ambalo linazikabili skuli nyingi hapa nchini. 


Baada ya hafla hiyo ya makabidhiano yaliyofanyika Skuli ya Mwanakwerekwe C Balozi aliwaambia walimu kuwa wanadhamana kubwa ya kuvitunza na kuvilinda ili viweze kusaidia kupunguza tatizo la upungufu wa vifaa vya sayansi . 

 Balozi Singal amesema kuwa tukitunza na kulinda vitasaidia na matunda yake yataonekana na ile taabu ya vifaa hivyo itakuwa imepunguwa 

 Naye Waziri wa elimu Zanzibar Ali Juma Shamhuna amevikabidhi vifaa hivyo kwa skuli sita kwa niaba ya skuli ishirini na sita zaambapo Unguja zitapata skuli 26 na Pemba skuli 16. Kwa Unguja ni pamoja na skuli ya Ben Bella Lumumba Mwanakwerekwe C Mkwajuni Nungwi na Tumbatu. 

Kwa upande wa Pemba bado hazijzjulikana ni skuli zipi zitakazofaidia na msaada huo. 

 Vifaa hivyo vinatokana na maombi ya aliyekuwa waziri wa elimu na mafunzo ya amali HaruoniAli Suleiman alipotembelea India katika ziara aliyokwenda na Rais Aman.

 Akitowa nasaha zake kwa walimu wakuu na wanafunzi waliohudhuria katika sherehe hiyo ya makabidhian Waziri wa elimu na mafunzo ya amali Ali Juma Shamuhuna amewataka wanafunzi kuacha tabia ya kukopia na kufanya udanganyifu kwani utazalisha watendaji wabovu wa baadaye. 

 Aidha amesema kuwa huu ni msaada ambao utapunguza sana upungufu wa vifaa vya sayansi na katika hali hii tutegemee matokeo mazuri katika masomo husika Alimhakikishia Balozi huyo kuwa vifaa ambavyo vimekabidhiwa kwa wizara ya elimu vitatumi,a kwa malengo yaliyokusudiwa na sio vinginevyo.  

 Imetolewa na Idara ya habari Maelezo Zanzibar

1 comment:

  1. Tunawashkuru sana hao ubalozi wa India kwa msaada wao lkn. mimi nadhani tatizo la masomo ya sayansi sio ukosefu wa vifaa peke yake bali ni usimamizi wa elimu kwa ujumla.

    Nilikua naangalia matokeo ya kidatu cha sita mda mfupi uliopita, kwa kweli matokeo ya Z'BAR yanaskitisha!..hata Lumumba iliyokua ikitutoa kimasomaso nayo hoi!

    Kwa kweli ndugu zetu UWAMSHO na hili watusaidie, waizindue SMZ na Wazazi juu ya umuhimu wa elimu kwa watoto wao!.. na sio tu kutuambia kua NECTA wanatuonea!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.