Habari za Punde

Kkosi cha Zimamoto Chazindua Kifaa Kipya DSPA 5


Kamishna Ali Abadalla Malimussa kushoto akiangalia kifaa kipya cha kuzimia moto kijulikanacho kama DSPA 5 kutoka kwa askari wa kikosi cha Zima moto na uokozi katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho Maisara mjini Zanzibar

Mkurugenzi wa mtendaji wa Kampuni ya Your Solution Tanzania LTD Damian George kushoto akimkabidhi kivaa kipya DSPA 5 Naibu Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Issa Haji Gavu katika hafla ya uzinduzi wa kifaa hicho Maisara mjini Zanzibar

Frans Volgelzangs ambaye ni mtaalamu wa Kampuni ya AFG inayozalisha kifaa kipya cha kuzimia moto ania ya DSPA5 akitoa maelezo jinsi ya kukitumia kifaa hicho. Picha zote na Iddi Haji-Maelezo Zanzibar Na

Ali Issa-Maelezo

 Kikosi cha Zima moto na uokozi Zanzibar (KZU) kimezindua kifaa kipya cha kisasa chakuzimia moto kiitwacho Dry Sprinkler Powder Aerosol (DSPA 5),ambacho huzima moto ndani ya dakika mbili baada ya kifaa hicho kukitumbua fyuzi zake kwa sekunde nane. 


 Uzinduzi huo umefanyika Maisara Mjini Zanzibar mbele ya Naibu Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Issa Haji Gavu pamoja na makamanda mbalimbali wavikosi vya SMZ na makamishina kutoka vikosi vyote.


 Katika uzinduzi huo Kamishina wa kikosi hicho Ali Abdalla Malimusa alisema kuwa kifaa hicho kimekuja wakati muafaka kwavile kumekuwa na matukio mbali mbali ya kuwaka kwa majengo ya Serikali, nyumba za watu binafsi na Ofisi za kiraia ,hivyo kifaa hicho kitakuwa muokozi wa maafa hayo iwapo yatatokea. 

Amesema Zanzibar ni Taifa linalohitaji mabadiliko ya kidunia ili kwenda sambamba na dhana za kisasa za uokozi pale ambapo pametokea janga la moto na kwamba hakuna budi kupambana nalo bila ya kuleta maafa . 

 “Nikifaa muhimu kwani hakitumii maji kitasaidia kwa kiasi kikubwa nchini kwetu kwani sisi ni sehemu ya dunia ”alisema Kameshina Ali Abdalla . 

 Nae Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya ‘Your Solution Tanzania LTD’ ambayo imeshirikiana na AFG Group ya Uholanzi Damian Geoge akitoa ufafanuzi wakifaa hicho cha DSPA alisema kuwa lengo hasa la kifaa hicho ni kuwaonesha Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla namna ya kukitumia pale litatokea janga la moto. 

Alisema DSPA ni tekinolojia ya kisasa ambayo haina madhara yoyote ya kiafya wakati wa uzimaji moto hata pale mtu atakapokuwa yupo ndani wakati wa kuzima moto . 

 Amesema kifaa hicho kwa nchi za Afrika, Tanzania imekuwa nchi ya kwaza kufika ambacho huzima moto kwenye chumba chenye ukubwa wamita 100 za mraba kwa Dspa 5 moja yenye uzito wakilo moja . Kifaa hicho kina uwezo wa kudumu kwa miaka 15 bila ya kuharibika baada ya kukinunua. 

 IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.