Habari za Punde

Mkutano wa Baraza la Wawakilishi na Kuapishwa Mhe. Raza wa Jimbo la Uzini.

Mwakilishi Mpya wa Jimbo la Uzini ndani ya Jumba akiwa katika viwanja vya Baraza akiingia kwa ajili ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini Mohammed raza Hassanali Darams.
Mjumbe wa Baraza Asha Bakari akiwa na Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed Raza Hassanali Darams, wakiteta jambo wakiwa ndani ya Ukumbi wa Mkutano kabla kuaza kwa kikao cha asubuhi na kuapisha kwake.
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho akiingia katika Ukumbi wa Mkutano wa Baraza la Wawakilishi kwa kuaza kwa kikao cha asubuhi na kumuapisha Mwakilishi wa Jimbo la Uzini.
Spika wa Baraza la Wawakilishi akisoma dua kabla ya kuaza kwa kikao cha baraza cha asubuhi.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi Mohammed raza Hassanali Darams, akila kiapo cha Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi Jimbo la Uzini, katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi. 
Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Ameir Kificho, akimpogeza Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed raza Hassanali Darams, kwa ushindi wa Chama chake na kuingia katika Baraza la Wawakilishi.  
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammed raza Hassanali Darams, akiwa na kabrasha lake baada ya kukabidhiwa na Spika akirudi sehemu yake ya kukaa. baada ya kumaliza taratibu za Ujumbe wa Baraza wa kula kiapo. 
Mwakilishi wa Uzini akiwa ameketi katika nafasi yake aliopangiwa katika Ukumbi huo na kuendelea na kikao cha asubuhi.
Wajumbe wa Baraza wakiendelea na Kikoa cha asubuhi baada ya kuapishwa mwakilishi wa jimbo la Uzini na kuendelea na maswali na majibu.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Mkoa wa Kusini Unguja na Wananchi wa Jimbo la Uzini waliomshindikiza katika sherehe za kuapishwa wakiwa nje ya jengo la Baraza Chukwani.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini akiwa na Kamati ya Maendeleo ya Jimbo la Uzini.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini akishindikizwa na Viongozi Chama Mkoa wa Kusini na Wananchi wa Jimbo la Uzini akitoka katika viwanja vya Baraza baada ya kuapishwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kupitia Chama cha Mapinduzi.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mohammedraza Hassanali Darams,akizungumza na Waandishi wa habari na Wananchi wa jimbo la Uzini katika ukumbi wa hoteli ya Turkey Malindi.
Mwakilishi wa Jimbo la Uzini akionesha barua kutoka Ubalozi wa Canada ya kueleza yeye siyo Raia wa Canada, kama baadhi ya watu waliokuwa wakisema ana uraia wa Nchi hiyo.wakati alipokuwa akizungumza na waandishi kutowa shukrani zake. 
Mwakilishi wa jimbo la Uzini akionesha risiti ya shilingi milioni 20, aliyolipia Idaraya Barabara kwa ajili ya kuziwekea kifusi barabara za jimbo hilo, mbele vya waandishi wa habari.   
Waandishi wa habari wakimsikiliza Mwakilishi wa jim,bo la Uzini akitowa maelezo jinsi ya ahadi zake alizoahidi kuaza kuzitekeleza.
Wananchi wa Wilaya ya Kati wakimsikiliza Mwakilishi wa Uzini akitowa maelezo yaahadi zake na jinsi ya kuaza kuzitekeleza katika jimbo hilo.

No comments:

Post a Comment

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.