Habari za Punde

Milioni 700 Kutumika Sherehe za Mapinduzi

Na Faki Mjaka-Maelezo Zanzibar

Zaidi ya Shs. Million 700 zinatarajiwa kutumika katika kuadhimisha Sherehe za miaka 48 ya Mapinduzi Zanzibar ambayo kilele chake kitakuwa Januari 12 Mwezi huu huko katika Uwanja wa Amani Mjini Zanzibar



Akitoa taarifa mbele ya waandishi wa habari leo huko ofisini kwake Vuga, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mohamed Aboud Mohamed amesema kuwa fedha hizo ni kwa makisio tu lakini taarifa kamili ya matumizi hayo itatolewa baada ya kukamilika kwa sherehe hiyo




Amesema kuwa sherehe za mwaka huu zitakuwa ni tofauti kidogo tu ukilinganisha na miaka iliyopita kwani wanafunzi hawatoshirikishwa wakiwa wamevaa sare zao kwani imeonekana kuwa wananchi wengi watahudhuria sherehe hizo.


Amesema kuwa Kiwanja kilichokuwepo kwa sasa hakikidhi haja ya kuweza kuwachukua wananchi wanaokadiriwa kuzidi uwezo wa uwanja huo ambao ni watu 15 Elfu tu.


Hata hivyo Waziri Aboud amesema kuwa Wanafunzi hawakatazwi kuja kusherehekea wakiwa wamevaliwa nguo zao kama wananchi wa kawaida


Akizungumzia suala la Sherehe hizo kuitwa za Mapinduzi wakati Zanzibar inaendesha Chaguzi zake kwa njia za kidemokrasia, amesema kuwa Neno Mapinduzi ni kitu ambacho kilichowagomboa wananchi wa Zanzibar kwa hivyo Serikali imeona iko haja ya neno hilo lienziwe kwani Mapinduzi ndiyo yaliyowagomboa Wananchi wa Zanzibar kutoka katika makucha ya Wakoloni.


Aidha amewapongeza wananchi wa Zanzibar pamoja na waandishi wa habari kwa mashirikiano yao makubwa ambayo wameyaonesha katika kusherehekea sherehe hizo za miaka 48 ya Mapinduzi tangu kuanza kwake tarehe 4 mwezi huu.


Waziri Aboud ametoa wito kwa wanachi kuhudhuria kwa wingi katika sherehe hizo ambazo milango yake itafunguliwa kuanzia saa 12 za asubuhi siku ya kilele

1 comment:

  1. Tizama ujinga huo hizo fedha zingetumika uwanja wa ndege wa zanzibar ndege hazitui usiku kwa sababu uwanja hauna taa, ndege nyingi hazitui kutokana na ubovu wa uwanja. kuliko kusheherekea kwa kuuliwa watu waliokuwa Innocent ndio maana nchi barka inaoondoka kazi yenu chuki husda. tizameni Dar uwanja mzuri kabisa ndege zote zinatuwa.na sasa hivi karibu wataanza ujenzi wa daraja la kigamboni.fanyeni maendeleo amkeni bado mmelala!!

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.