Habari za Punde

DK. SHEIN AKIWA KATIKA ENEO LA TUKIO NUNGWI AKIJUMUIKA NA WANANCHI KUPOKEA MAJERUHI NA MAITI

































 MMOJA wa Abiria aliyekuwa katika ajali hiyo Khamis Jabu Faki (62) akizungumza na Mwandishi wa Redio Zenj Fm Hafidh Kassim baada ya kufikishwa katika ufukwe wa pwani ya Nunwi akielezea jinsi ya ajali ilivyotokea.

 WANANCHI wa Kijiji cha Nungwi wakiwa ufukweni mwa Bandari ya Nungwi wakiwasiliana na waokoaji wakiwa baharini.
 MAJERUHI  wa ajili ya Meli ya Spice wakipata huduma ya kwanza baada ya kuwasal katika bandari ya Nungwi baada ya kunusurika. 


 WANANCHI wakiwa katika Ufukwe wa Bandari ya Nungwi kuwatambua watu wao
 MOJA ya boti inayoopowa maiti na majeruhi ikiwa na miili ya watu waliokufa katika ajali ya meli ikiwa katika bandari ya Nungwi. 
 HALI ya uokoaji ikiendelea katika pwani ya Nungwi.
 WANANCHI  na Askari wa Vikosi vya Ulinzi wakiwa na miili ya marehemu  wakiitowa katika boti za uokoaji bandari ya Nungwi.
 ASKALI wa Jeshi la Wananchi wakitowa msaada wa katika zoezi hilo la uokoaji wakiwa katika  bandari ya Nungwi. 
 WATALII kutoka Nchi Ufaransa wakitowa huduma ya kwanza kwa majeruhi wa Meli ya Spice iliozama katika Mkondo wa bahari ya Nungwi.
 MSAADA hutolewa popote ndivyo inavyoonekana Watalii  kutoka Ufaransa wakitowa huduma ya kwanza kwa majeruhi

 MTALII kutoka Ufaransa Jullie akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa mtoto aliyenusurika katika ajali ya Meli ya Spice baada ya kuokolewa wakiwa katika bandari ya Nungwi.
MWANDISHI wa habari gazeti laZanzibar Leo Ramadha Makame akimuhoji mmoja wa majeruhi wa ajali hiyo katika ufukwe wa bahari ya Nungwi

3 comments:

  1. Serikali lazima iwaeleze wananchi kwanini imeruhusu boti mbovu kuwa imejaza kupita kiasi.kwa uroho wa fedha na rushwa kwa wachache. kwanini serikali imeshindwa kutafuta boti za uokozi haraka?

    ReplyDelete
  2. Uombozi wa siku tatu hausaidii chochote serikali lazima ikubali jukumu,Wawalipe fidia walioathirika na waliohusika na uzembe huu lazima washtakiwe.

    ReplyDelete
  3. Namuunga mkono comments za wenzangu waliotangulia ila mimi naomba niwe tofauti kidogo.Katika hili serikali inatakiwa kujibu maswali yafuatayo:
    1)Kwanini iliruhusu boti kujaza abiria na mizigo kupita kiasi? (ubovu hatuna hakika na hata ingekua mpya kwa mzigo ule isingetoka)
    2)Kwanini juhudi za uokozi zilichelewa sana na zikawa duni?
    4)Kwanini SMZ isinunue meli kubwa za abiria na mizigo kama vile MV.Mapinduzi na Maendeleo, hiyo ni biashara kwa serikali kama ikisimamiwa vizuri (Inaonekana hakuna mfanyabiashara anaeweza kununua meli hapa ni maboti tuu tena yaliyochoka!)
    3)Na kwa nini wanaosababisha uzembe wa namna hii(kuruhusu vyombo kujaza kupita kiasi) hawachukuliwi hatua ikawa mfano kwa wengine? Ama kuhusu suala la watu kulipwa fidia na mimi nigedhani hivyo kama ningekua sielewi hali halisi ya uchumi wa Zanzibar.Tukubaliane SMZ ilikua holidays kwa muda mrefu, ndio kwanza "inakumbuka shuka" asubuhi hii!
    Mungu azilaze roho za marehemu wetu peponi na atupe subra sisi tuliobaki.Inna Lil- Lahi,Wainna Ilaihi-Rajiuun.

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.