Habari za Punde

MAZISHI YA MUFTI KATIKA PICHA

Baadhi ya Viongozi waliohudhuria mazishi.
Mtangazaji wa Radio Al noor, akitangaza moja kwa moja kutoka katika eneo la makaburini alikozikwa Mufti wa Zanzibar.



Balozi Mdogo wa Oman aliyeko Zanzibar akitabaruku kuweka mchanga kaburini.
Wananchi waliohudhuria mazishi ya Mufti wa Zanzibar wakiitikia duwa.
Kadhi Mstaafu Habibu Ali Kombo akisoma duwa katika kaburi la Marehemu Mufti wa Zanzibar baada ya maziko yake yaliofanyika huko kijijini kwao Muyuni.
Shekhe Mussa Soraga, Kiongozi wa kamati ya Maziko, akisoma wasifu wa Marehemu Mufti wa Zanzibar Shekhe Harith bin Khelef baada ya kufanyika maziko yake huko kijijini kwao Muyuni Mkoa wa Kusini Unguja.
Makamo wa Rais wa Tanzania Dk. Ali Mohammed Shein akimfariji ndugu wa marehemu Mufti wa Zanzibar huku kijijini kwao Muyuni baada ya kumalizika mazishi ya Mufti wa Zanzibar Alhaj Harith bin Khelef.
RAIS Mstaaf Ali Hassan Mwinyi akimfariji ndugu wa marehemu Mufti wa Zanzibar huko kijijini kwao Muyuni Zanzibar, baada ya mazishi kufanyika.
WAZIRI Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha akimfariji Dada wa Marehemu Bi Moza Khelef, nyumbani kwake katika kijiji cha Muyuni Wilaya ya Kusini Unguja alikozikwa Mufti wa Zanzibar.
Askofu Mkuu wa Kanisa la Anglikana Agustino akimfariji mmoja wa wanandugu wa Marehemu Mufti Harith bin Khelef aliyezikwa kijijini kwao Muyuni mkoa wa kusini Unguja.
Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Shaaban Bin Simba akiongoza Du'aa kumuombea Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Harith bin Khelef wakati mwili wake ulipowasili katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere. Kulia kwa Mufti ni Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi na anaefuatia ni Kaimu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis. Kushoto kwa Mufti ni Sheikh Mkuu wa Dar Al Had Musa Salum.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Amani Abeid Karume (wa tano kushoto) alijumuika na Viongozi wengine katika swala ya Maiti ya Marehemu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Harith Bin Khelef katika Msikiti wa Mwembeshauri jana.Maelfu ya wananchi na waumini wa dini ya kiislamu wakiubeba mwili wa marehemu Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Harith bin Khelef aliyefariki Nchini India na kuzikwa jana kijijini kwao Muyuni, Wilaya ya Kusini Unguja.

2 comments:

  1. Innaa lillaahi Wainnaa Ilayhi Raajiuun

    InshaAllah Mwenyezi Mungu akipokee kiumbe chake kwa mapokezi mema na amsamehe makosa yake.

    ReplyDelete
  2. “Innaa lillahi wainnaa ilayhi raajiuun”
    Truly ! to Allah we belong and truly, to him we shall return”

    ReplyDelete

ZanziNews Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.